Monday, May 27, 2013

Zidane apewa kazi ya kumpeleka Bale Real Madrid

Wanted: Gareth Bale
Baada ya Barcelona kufanikiwa kumsajili Neymar, klabu ya Real Madrid imeweka nguvu zake zote kuhakikisha Gareth Bale wa Tottenham anasajiliwa kwa gharama yoyote. Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa klabu ya Real Madrid imempatia kazi hiyo Zinedine Zidane ambaye ni moja ya washauri wa Madrid kwenye masuala ya usajili. Zidane amepewa bajeti ya paundi mil 65 ili kuhakikisha Bale anajiunga na Madrid. Zidane  alipoulizwa na gazeti la Marca kuhusiana na jambo hili alikiri kuwa ni kweli na zaidi alisema “ Nimekuwa naishauri Madrid kwa kipindi kirefu, na kwasasa nimewashauri wamsajili Bale kwasababu ni mchezaji anayefuatia baada ya Messi na Ronaldo kwenye soka la dunia hivi sasa, ana kasi, na kiwango chake hakitegemei mechi, kila mechi kiwango chake kipo vilevile, hivyo ni kazi yangu kufanikisha Bale anasajiliwa na Madrid”. Mpango huu wa Madrid ukifanikiwa kwa kumsajili Bale, basi ada ya uhamisho wake ndiyo inatabiriwa kuwa kubwa kuliko zote kwenye msimu huu wa usajili. 

No comments:

Post a Comment