Thursday, May 9, 2013

TFF,vyama vya mikoa viendelee na Copa Coca cola

Vyama vya Mpira wa Miguu vya mikoa vinatakiwa na TFF kuendelea na mashindano ya Copa Coca-Cola yanayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 katika ngazi ya wilaya wakati vikisubiriwa vifaa na fedha za uendeshaji kutoka kwa mdhamini. Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano (roadmap), mashindano ya Copa Coca-Cola ngazi ya wilaya yanatakiwa kufanyika na kukamilika ndani ya mwezi Mei mwaka huu ili baadaye kuendelea na hatua inayofuata. Hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka wanachama wake (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa) ambao wamejipanga kuendelea na mashindano wakati suala la vifaa na fedha likiendelea kufuatiliwa kwa mdhamini wa mashindano. Vifaa na fedha zitapatikana wakati wowote baada ya taratibu husika kukamilika. Vifaa kwa ajili ya mashindano hayo vimeagizwa kutoka nje ya Tanzania. Ni matumaini yetu kuwa tutakuwa na mashindano mazuri mwaka huu kulinganisha na msimu uliopita. Kampuni ya Coca Cola ilianza kudhamini mashindano hayo mwaka 2007, na tangu mwaka huo yamekuwa yakifanyika kila mwaka.

No comments:

Post a Comment