Mshambuliaji wa Man utd Wayne Rooney amebadilisha msimamo wake wa kutaka kuhama United baada ya kusikia kocha wake wa zamani David Moyes anatarajiwa kujiunga na United. Rooney alikuwa chini ya kocha David Moyes kwa kipindi cha miaka miwili alipokuwa mchezaji wa Everton, na Moyes ndiye aliyemfanya Rooney aonekane hadi kusajiliwa na Man utd. Moyes alikuwa akimpenda Rooney na kuweza kumpanga kwenye kikosi cha kwanza kila mechi hadi alipoondoka kwenda United. Rooney amebadilisha kauli yake kwani mwishoni mwa mwezi uliopita alimwambia Sir Alex kuwa msimu ujao ataihama United licha ya kuwa Sir Alex alimkatalia, hali hiyo ilileta mtafaruku baina ya Rooney na Sir Alex lakini baada ya Sir Alex kutangaza kuachia ngazi na nafasi yake kusemekana itachukuliwa na Moyes ndipo Rooney akatangaza kuwa hawezi tena kuondoka United kwasababu Moyes anarudi.
Manchester mbioni kumrudisha Cristiano Ronaldo
Wakati huo huo David Gill mkurugenzi mtendaji wa United wiki hii alikwenda nchini Hispania kukutana na wakala wa Ronaldo kuongea naye ili kumrudisha Ronaldo ndani ya kikosi cha United, habari hizi zimethibitishwa na Sportmail na kuongeza kuwa, hii ni mojawapo ya sababu ya Rooney kubaki United kwani Cristiano alikuwa ni mchezaji wanayeshirikiana vyema wakiwa ndani ya uwanja. Ikumbukwe Wayne Rooney alikuwa akicheza kama mshambuliaji wa mwisho lakini tokea msimu huu uanze Rooney amekuwa akicheza nafasi ya kiungo jambo linalomfanya ashindwe kucheza vizuri ndiyo maana akapata hamasa ya kutaka kuhama kwenda PSG ya Ufaransa alipokuwa Muingereza mwenzake David Beckham.
No comments:
Post a Comment