Tuesday, June 25, 2013

Ancelotti kocha mpya Madrid na Blanc atua PSG

Carlo Ancelotti ametangazwa rasmi kuchukua mikoba ya Jose Mourinho ya kuifundisha klabu ya Real Madrid akitokea PSG ya Ufaransa. Ancelotti amesaini mkataba wa miaka mitatu na Madrid na anatarajiwa kutambulishwa rasmi jumatano ya kesho kwa waandishi wa habari. Kabla ya kujiunga na Madrid, Ancelotti ameshawahi kufundisha klabu za Juventus, Milan, Chelsea na PSG.
Laurent Blanc: Future to be decided within 48 hours
Baada ya Ancelotti kuondoka PSG, klabu hiyo imemtangaza Laurent Blanc (kwenye picha) kama kocha mkuu wa klabu hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na anatarajia kuanza kazi rasmi Julai 1. Kabla ya kujiunga na PSG, Blanc ameshawahi kufundisha timu ya Bordeaux na timu ya taifa ya Ufaransa. 

No comments:

Post a Comment