Tuesday, June 25, 2013

Schurrle wa Leverkusen atua Chelsea

Schurrle
Klabu ya Chelsea imefanikiwa kumsajili rasmi mshambuliaji wa Bayern Leverkusen Andre Schurrle kwa ada ya paundi mil 18. Schurrle (22) amesaini mkataba wa miaka mitano utakaodumu hadi mwaka 2018. Shurrle alipohojiwa baada ya kusaini mkataba na Chelsea alisema 'nimefurahi kujiunga na Chelsea, ni klabu kubwa, sikuwahi kufikiria kucheza kwenye klabu hii, namshukuru Jose Mourinho kwa kunichagua mimi, nilikutana naye kwa mara ya kwanza mwaka huu nchini Ujerumani kwenye mechi ya kirafiki, tukasalimiana na aliniambia kila kitu kimekwenda vyema kuhusu usajili wangu na nitarajie kujiunga na Chelsea, hivyo leo ahadi yake imetimia na mimi natoa ahadi kwake na wapenzi wote wa Chelsea kuwa nitacheza kwa bidii ili kushinda vikombe'. Schurrle alijiunga na Leverkusen mwaka 2011 na amefanikiwa kucheza mechi 65 na kufunga magoli 18 kwa kipindi chote akiwa ndani ya klabu hiyo.

Signed on the dotted line: Andre Schurrle has penned a five-year-deal and will wear the No 14 shirt

No comments:

Post a Comment