Tuesday, June 4, 2013

Drogba kakataa kuja timu ya taifa-Lamouchi

Kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi amesema sio kweli kuwa yeye ndiye sababu ya Drogba kutokuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa. Lamouchi amesema “Drogba aliniambia mwenyewe kuwa kwasasa anataka kupumzika kucheza kwenye timu ya taifa kwasababu anahisi kiwango chake kimeshuka na anahitaji muda kurudi kwenye kiwango chake ila tumepanga kumuita tena kwenye mechi ya kirafiki mwezi wa nane kama atakubali, ila sisi bado tunamuhitaji sana, ana mchango mkubwa sana kwenye timu yetu hata kama umri wake umekwenda”. Didier Drogba alicheza kwa mara ya mwisho kwenye timu ya taifa mwezi februari mwaka huu 2013 kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Afrika ya kusini na alikosa mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Gambia na vilevile haijatwa kwenye kikosi kitakachocheza wikiendi hii dhidi ya Gambia na atakosa pia mechi dhidi ya Tanzania.  

No comments:

Post a Comment