Tuesday, June 4, 2013

Kesi ya Pistorius yasogezwa mbele kwa uchunguzi

Mwanariadha wa Afrika ya Kusini Oscar Pistorius leo amepandisha tena kizimbani jijini Pritoria na mahakama imeomba kesi yake isikilizwe tena mwezi wa nane mwaka huu ili kutoa muda wa kufanya uchunguzi zaidi. Bwana Pistorius anakabiliwa na kesi ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi kitendo ambacho mtuhumiwa alikitenda usiku wa tarehe 14 mwezi Februari mwaka huu akiwa nyumbani kwake. Mahakama imepeleka mbele kesi hiyo kwasababu alizozitoa Oscar kuwa alimuua mpenzi wake akidhani ni jambazi aliyetaka kumdhuru, hivyo alimfyatulia risasi ili kujikinga. Kufuatia kesi hii Pistorius ametangaza kusimama kushiriki michuano yoyote mwaka huu hadi hapo mahakama itakapotoa hukumu ya kesi yake. 

Delayed: Pistorius murder trial was postponed until August

No comments:

Post a Comment