Thursday, July 18, 2013

Azam FC yamponda na kumtema rasmi Humoud

Abdulhalim Humoud
Kumekuwa na minong'ono kwenye vyombo vya habari kuhusu usajili wa mchezaji wa Azam Fc Abdulhalim Humoud kwenda Jomo Cosmos Fc ya Afrika Kusini kuwa umehujumiwa na klabu yake. Humoud amekuwa akiilalamikia klabu yake ya Azam Fc kuwa imesababisha usajili wake kwenda Jomo kusuasua kwa sababu zisizoeleweka. Homoud alisikika kwenye radio na magazeti akitoa malalamiko yake kwa klabu ya Azam Fc, lakini leo klabu ya Azam Fc pia imeeleza ukweli kwa upande wake. Taarifa hizi za Azam Fc zimetolewa bila kutaja jina la mchezaji huyo lakini zikiwa wazi kumlenga Humoud kama zilivyonukuliwa hapo chini;  


1.Ana Barua Mkononi aliyopewa na Uongozi wa Azam Kumfahamisha kuwa yupo huru kujiunga na Jomo Cosmos,

2.Ana mkataba mkononi aliosaini kati yake na Jomo Cosmos

3.Azam FC wameshamwaga wino kwenye transfer contract kumruhusu akajiunge na Jomo Cosmos on free transfer tangia April 2013

4.Analalamika eti Azam FC inatangaza kumuondoa kwenye usajili kwa kuwa ameuzwa South Afrika badala ya kufurahi

5.Analalamika eti Azam FChaijamsafilisha… tangia lini uliona timu inayomuuza mchezaji inamsafirisha? Kimsingi wa kuulizwa ni Jomo Cosmos kwa nini hawatumi ticket

6.Muda wa usajili bado unaendelea tena unafungwa Septemba yeye analalamika kwenye vyombo vya habari badala ya kwenda klabuni kuuliza hatma yake.

7.Ili kumpa uhuru wa 100% Azam FC leo imeamua kumlipa kilichobaki kwenye mkataba wake na kuachana naye ili kumpa uhuru kamili… sasa ni mchezaji huru… wanaosema Azam FC inambania sijui wanatoa wapi hizo hoja? Mbaya zaidi hata wale waliomhoji hawajathubutu kutafuta ukweli upande wa pili… hii yote inaonesha kuwa waliomhoji walikuwa na lao jambo au hawajui misingi ya objective jounalism ambapo kama mwandishi ni lazima uweke habari yako kwenye mizania kwa kuhoji pande zote mbili

8.Tunamtakia kila la kheri Abdulhalim Humoud katika maisha yake kama mchezaji huru 100%

Haya ni maneno ya Azam FC iliyoyatoa leo kuhusu Humoud

Huu ndiyo mkataba wa Humoud na Jomo uliotolewa na Azam Fc ili kuthibitisha kumruhusu mchezaji huyu kwenda Jomo

No comments:

Post a Comment