Kocha mpya wa klabu ya Barcelona, Gerardo Martino 'Tata' anatarajia kuanza kazi ijumaa ya wiki hii baada ya kutambulishwa rasmi na kusaini mkataba. Martino anayechukua nafasi ya Tito Vilanova, anatarajia kuwasili jijini Barcelona Alhamisi ya tarehe 25 ambapo atatembelea sehemu mbalimbali za klabu hiyo na kupiga picha maalumu za ukaribisho, na siku ya ijumaa atasaini mkataba na kuongea na waandishi habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo. Katika mahojiano ya kwanza na waandishi wa habari akiwa Argentina, Martino alisema ' nimefurahi kupata nafasi ya kuifundisha klabu kubwa kama Barcelona, sikuwahi kufikiria hili, ila naamini Messi na Baba yake wanamchango mkubwa katika uchaguzi wangu, hivyo nawashukuru kwa kuonesha imani na mimi. Nimekuwa mpenzi wa mfumo wa Barcelona tokea siku nyingi, na huu ni wakati mzuri kwangu kuuendeleza. Nakwenda Ulaya kuanza kibarua kipya na Barcelona, najua Ulaya kuna changamoto nyingi lakini naamini nitaweza kuzikabili kadri ya uzito wake'. |
Wednesday, July 24, 2013
Gerardo Martino 'Tata' kuanza kazi rasmi ijumaa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment