Thursday, July 11, 2013

Guardiola ameanza kuwafundisha Bayern Tiki-Taka

Kocha mpya wa Bayern Munich, Pep Guardiola ameanza kwa kasi kuwapa mazoezi wachezaji wa klabu hiyo ili kutimiza ahadi aliyoitoa siku za mwanzo. Guardiola alitoa ahadi ya kuwafundisha wachezaji wa Bayern Munich kucheza Tiki-Taka mfumo unaochezwa kwa pasi fupi na kumiliki mpira kwa muda mrefu. Klabu ya Barcelona ndiyo waasisi wa mfumo huu na Pep Guardiola aliiwezesha vyema klabu ya Barcelona kung'aa kwa kutumia Tiki Taka na ndiyo sababu kubwa ya uongozi wa Bayern Munich kumpatia kazi Pep ya kuwafundisha wachezaji wa klabu hiyo filosofia hii ya Tiki Taka. Katika kufanikisha hili, Pep ameshaanza kuwafundisha wachezaji wa Munich mfumo huu, licha ya kuwa ulionekana kuwa mgumu siku za mwanzo kwa wachezaji wa Munich kujifunza, lakini kadri siku zinavyokwenda imeonesha wachezaji wameanza kumuelewa Pep. Wachezaji wa Munich wamebakiza mwezi mmoja tu kuuelewa mfumo huu kabla ya ligi kuu ya Ujerumani kuanza. Lakini tarehe 24 mwezi huu (Julai) klabu ya Bayern Munich itacheza mechi ya kirafiki na klabu ya Barcelona mchezo utakaotumika kwa Bayern kujipima kiwango chao cha Tiki Taka.   

Video hii inaonesha Guardiola akiwa kwenye hatua za mwanzo kuwafundisha mfumo wa Tiki Taka wachezaji wa Bayern Munich

Pointing the way: Guardiola knows what he wants, and how to get it
This is how you do it: Alaba receives a lecture from the boss
Masterplan: Guardiola speaking to star winger Arjen Robben
Fantastic view: The players were training in the picturesque town of Arco in ItlayNot going anywhere: Kroos holding back Ribery by the shirt

No comments:

Post a Comment