Wednesday, June 26, 2013

Azarenka ajitoa Wimbledon baada ya kuumia

Mcheza tenesi namba mbili duniani kwa upande wa wanawake Victoria Azarenka amejitoa kwenye michuano ya Wimbledon baada ya kuumia kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Maria Joao Koehler. Azarenka aliumia baada ya kuteleza na kupiga msamba kwenye seti ya pili licha ya kuwa alijitahidi na kufanikiwa kushinda mechi hiyo. Baada ya tathimini ya daktari wake, Azarenka leo ametangaza kujitoa kwenye michuano hiyo ili aweze kupata matibabu ya kutosha. Azarenka alitakiwa kukutana na Flavia Pennetta kwenye raundi ya pili, lakini kwa kujitoa kwake kunamfanya Flavia afuzu hadi raundi ya tatu. 

Painful: Victoria Azarenka slipped over on the baseline against Maria Joao Koehler
Scary: Azarenka looked to be in agony at the back of the court
Victoria Azarenka injured
Azarenka akiwa amelala chini huku akiugulia uchungu baada ya kuteleza kwa kupiga msamba. Pole sana!!!!

No comments:

Post a Comment