Sportsmail linaripoti kuwa kocha mpya wa Barcelona, Gerardo Martino ' Tata' ameshapeleka maombi kwa uongozi wa klabu hiyo ya kutaka kumsajili wa beki mmoja . Martino amewataja mabeki watano kutoka ligi kuu ya Uingereza ambao ni Kompany (Man city), Luiz (Chelsea), Vertonghen (Spurs), Agger (Liverpool) na Vermaelen (Arsenal) ambapo mmoja kati ya hawa ndiyo ameombwa na kocha Martino asajiliwe. Klabu ya Barcelona ilishaanza kuongea na klabu ya Chelsea tokea mwezi wa tano ili kumsajili Luiz, lakini mazungumzo yaliishia njiani baada ya Mourinho kurudi Chelsea. Jose Mourinho alikatisha mazungumzo hayo baada ya kuuomba uongozi wa Chelsea usimuuze mchezaji huyu. Mategemeo ya Barcelona kwa awamu hii ya pili ni kuanza kuongea tena na klabu ya Chelsea ili kuangalia uwezekano wa kumsajili Luiz kwani ndiye chaguo la kwanza la kocha Martino. Taarifa zinasema Barcelona watahamia kwa mabeki wengine pindi Chelsea watakapogoma kabisa kumuachia Luiz. Barcelona inahitaji kusajili beki mmoja ili kuimarisha safu yake ya ulinzi iliyokuwa dhaifu msimu uliopita ikichangiwa na Abidal, Puyol na Pique kuwa majeruhi kwa muda mrefu. |
Tuesday, July 30, 2013
Mabeki watano waingia kwenye rada ya Barcelona
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment