Monday, May 13, 2013

Brian Kidd kushika nafasi ya Mancini kwa muda

Brian Kidd anatarajiwa kushika nafasi ya Mancini katika mechi zilizobakia kwenye ligi kuu baada ya uongozi wa klabu hiyo kutangaza nia yake ya kumfukuza kazi Mancini. Uongozi wa Man city umechukua uamuzi huo kwasababu Mancini ameshindwa kutimiza malengo ya mwaka ya klabu hiyo ikiwemo kutetea ubingwa wa ligi na kufika hatua ya robo fainali kwenye UEFA champions. 

Time's up: Roberto Mancini's spell as Manchester City manager will be ended this week

Kufuatia hatua hii wadau wengi wa soka nchini Uingereza wamehoji uamuzi wa klabu hiyo wa kumfukuza Mancini kwani wanaamini Man city imefanya vizuri mwaka huu licha ya kuwa haijaweza kushinda kombe lolote. Hoja ya wadau hao ni kwamba, timu zote za Uingereza msimu huu zimefanya vibaya kwenye UEFA, hivyo kigezo cha UEFA sio cha kumfukuza kazi Mancini, vilevile, Man city imefanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye ligi na kufikia hatua ya fainali FA cup kitu ambacho ni mafanikio makubwa kwa klabu kwani kuna vilabu vingine kama Arsenal, Chelsea na Liverpool havijaweza kufikia hatua ya Man city lakini vinajivunia nafasi zao. Vilevile, kwa upande mwingine baadhi ya wadau walisema ni haki kufukuzwa Mancini, kwasababu gharama ya uwekezaji na uendeshaji wa timu ya Man city ni kubwa kulinganisha na klabu zingine za England kwahivyo ilikuwa ni lazima kushinda kombe la ligi na kufika mbali kwenye UEFA champions ili kurudisha faida kidogo, kinyume cha hapo inakuwa ni hasara kwa timu. Hayo ni maoni tu ya wadau wa soka, lakini mwisho wa siku uongozi wa Man city ndiyo umeshapembua na kuona hafai.  

No comments:

Post a Comment