Saturday, July 20, 2013

Tetesi zimeanza za atakayekuwa kocha wa Barca

Andre Villas-Boas cools Barcelona talk after Tito Vilanova steps down as coach
Baada ya kocha wa Barcelona Tito Vilanova kutangaza kuachia ngazi, tayari majina ya makocha yameanza kutangazwa kuchukua nafasi ya hiyo. Moja ya makocha hao ni Andre Villas Boas ambaye ni kocha wa Tottenham, Juan Francesc Ferrer, 'Rubi' ambaye ni kocha msaidizi wa Barcelona hivi sasa na Michael Laudrup kocha wa Swansea aliyewahi kuichezea Barcelona wakati akicheza soka na Luis Enrique ambaye aliwahi kuwa kocha wa Barcelona B na mchezaji wa Barcelona. Andre Villas Boas alipoulizwa kuhusiana na nafasi hii ya kuifundisha Barca alisema ' kwasasa ni mapema sana kuongelea jambo hili, ni vyema kumtakia afya njema Tito Vilanova kuliko kuongelea nafasi yake'. Mbali ya AVB, makocha wengine ambao wametajwa kuziba nafasi hiyo, pia walikwepa kuongelea kuziba nafasi hiyo, wakisema wanamtakia afya njema Tito. Lakini historia na utamaduni wa klabu ya Barcelona unaonesha mtu atakaye kuwa kocha wa klabu hiyo ni lazima atoke kwenye familia ya Barcelona (awe amewahi kuchezea Barca au alishawahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo kwenye nafasi tofauti za timu au utawala) hivyo kwa mazingira haya, makocha wasaidizi wa Barca na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo ndiyo wenye nafasi kubwa ya kuchaguliwa kuiongoza Barca. Uongozi wa Barcelona kupitia Rais wake Rosell umesema hautachukua muda kumtangaza kocha mpya, na wanatarajia kumtangaza jumatatu au jumanne ijayo.  

Luis Enrique 
Juan Francesc Ferrer, 'Rubi' 

No comments:

Post a Comment