Saturday, July 20, 2013

Viingilio kombe la dunia, bei ya chini ni dola 90

FIFA World Cup tickets to go on sale
Kuelekea kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014, shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limetangaza viingilio vya mechi mbalimbali ya michuano hiyo. Viingilio hivyo vimegawanywa kwenye makundi mawili tofauti. Kundi la kwanza ni bei za tiketi kwa wazawa (Wabrazil) na kundi la pili ni kwa watu wa mataifa mbalimbali nje ya Brazil. Kwa wazawa tiketi zitaanzia dola 15 kwenye hatua ya makundi na kwa watu wa mataifa mengine tiketi zitaanzia dola 90 kwa hatua ya makundi. Mechi ya fainali tiketi zitauzwa kuanzia dola 442 hadi 990. Bei hizi zimetangazwa leo jijini Sao Paulo nchini Brazil na tiketi zitaanza kuuzwa tarehe 20 mwezi Agosti 2013 kwenye sehemu tofauti zitakazo tangazwa ikiwemo tovuti ya FIFA. FIFA inatarajia kuuza jumla ya tiketi milioni 3 kwenye mechi zote za michuano hii.  

No comments:

Post a Comment