Wednesday, August 14, 2013

'Sitavaa tena jezi za Tottenham Spurs'- Bale

Bale: I'll never play for Spurs again
The Sun linaripoti kuwa mshambuliaji wa Tottenham Gareth Bale amewaambia wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Wales kuwa hatavaa tena jezi ya Tottenham na anaamini atajiunga na Madrid msimu ujao. Bale amesema mechi iliyopita ndiyo ilikuwa ya mwisho kwake kuichezea Tottenham na anatarajia kuhamia Madrid licha yakuwa bado hajaelewa kwanini klabu yake hadi sasa imeshindwa kukubaliana na Madrid. Usajili wa mchezaji huyu kwenda Real Madrid umeshindika hadi sasa kwasababu Tottenham wanahitaji walipwe Euro 100mil, pesa ambazo Rais wa Madrid, Perez, amesema ni nyingi. Lakini maneno ya Bale kusema hataichezea tena Spurs ni ishara kuwa Madrid na Tottenham wamekaribia kufikia muafaka. 

No comments:

Post a Comment