Juan Mata ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari na jezi yake imeonekana ikiwa na namba 8. Jana ripoti zilitoka kuwa Mata atavaa jezi namba 7, lakini leo mambo yakaonekana tofauti. Fununu za vyombo vya habari nchini Uingereza zimesema, Mata alikataa namba 7 ambayo ilikuwa imendaliwa kwa ajili yake. Inawezekana kuwa Mata aligoma kuvaa namba 7 kutokana na ukubwa namba hiyo ambayo ilishavaliwa na magwiji mbalimbali waliowahi kuichezea Man utd akiwemo Cristiano Ronaldo, Best, Beckham na Cantona. Uamuzi huu wa Mata kuvaa jezi namba 8 utamfanya asiwe na presha kubwa ya kukidhi mategemeo ya mashabiki wa Man utd ambao wangetegemea kiwango kile kile walichokuwa nacho wachezaji wengine waliowahi kuvaa jezi hiyo.
No comments:
Post a Comment