Wednesday, August 14, 2013

'Sina mpango wa kurekebisha meno yangu' - Dinho

Ronaldinho
Mshambuliaji mkongwe wa Brazil Ronaldinho Gaucho akiongea na jarida la michezo la nchini Ufaransa 'So foot' amesema hana mpango wa kurekebisha meno yake kwani ndiyo utambulisho wa sura yake kwa watu. Ronaldinho ameyasema hayo baada ya kuulizwa na muandishi wa habari 'kwanini usirekebishe meno yako yakae vizuri', Ronaldinho akasema ' siwezi kubadilisha meno yangu kwasababu ndiyo utambulisho wangu'.  Meno ya Ronaldinho yalikuwa yanaonekana kituko enzi zile alipokuwa ameanza kujulikana, lakini baada ya kupata jina meno yake yamekuwa ni kivutio cha wengi katika kumtambua kama yeye mwenyewe alivyoelezea. Mcheki kwenye picha ya chini aliyovyotokelezea na meno yake :)
Ronaldinho

No comments:

Post a Comment