Sunday, August 18, 2013

Wachezaji wanne kugombania nafasi Barcelona

Four players fight for one place
Hakuna ubishi kuwa ujio wa Neymar utawafanya wachezaji wanne wa klabu ya Barcelona kugombania nafasi mbili. Alexis, Fabregas, Pedro na Tello wote hawa watakuwa wanapokezana nafasi mbili za kucheza kwenye ushambuliaji au winga. Kati ya wachezaji hawa, Alexis ndiye anapewa nafasi kubwa ya kucheza mechi nyingi kutokana na kiwango kizuri alichokionesha kwenye mechi za kirafiki kabla ya ligi kuanza. Pedro na Fabregas wanatarajiwa kuwa benchi kwenye mechi za mwanzo kutokana na majeraha waliyoyapata hivi karibuni, wakati, Tello ndiye anaonekana kuwa ni chaguo la mwisho la Tata kati ya wachezaji hawa kutokana na uzoefu wake mdogo alionao kwenye kikosi cha kwanza. Utabiri wa kikosi cha kwanza cha Barcelona ni 1. Valdes 2. Alves 3. Alba 4. Pique 5. Mascherano 6. Busquets 6. Xavi 7. Pedro 8. Iniesta 9. Alexis 10. Messi 11. Neymar .  

No comments:

Post a Comment