Azam FC na Simba zitakutana katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) kila moja ikisaka pointi za kujiweka vizuri kwenye ligi kuu ikiwa imesalia michezo michache kumalizika. Endapo Azam FC itashinda mchezo wa leo itafikisha pointi 49 ambazo haziwezi kufikiwa na Simba hivyo Kagera Sugar itabaki kama timu pekee inayoweza kufikisha pointi 49. Azam FC inaizidi Kagera Sugar magoli 14 idadi ambayo ni ngumu kwa kagera kuigeuza kwa mechi nne zilizosalia. kwa maana hiyo Azam FC itakuwa imejihakikishia nafasi ya pili na kutimiza malengo yake iliyojiwekea msimu huu. Akizungumza kupitia mtandao wa AZAM FC, kocha Stewart amesema ameandaa kikosi maalum cha kuikabili Simba kwa kuwa anajua watachezesha wachezaji wao muhimu katika mchezo wa leo utakaobadilisha muonekano wa ligi kuu. “Ni mchezo mgumu wote tunatafuta pointi, naimani wachezaji wangu watafanya vizuri kutokana na maandalizi tuliyofanya" amesema Stewart. Baada ya ja Simba kuvuliwa ubingwa na Yanga, timu ya Simba leo itainga uwanjani muda mfupi ujao kupambana na Azam FC katika mchezo utakaokuwa ni mkali. Endelea kutembelea MichezoUpdates kupata matokeo ya mchezo wa leo
No comments:
Post a Comment