Tuesday, October 8, 2013

Arsenal yapata tuzo mbili kwa mpigo

Double recognition: Ramsey and Wenger are presented with their awards at Arsenal's London Colney training ground
Arsenal boss, Arsene Wenger na kiungo Aaron Ramsey wakionesha tuzo zao walizozipata baada ya kuchaguliwa kuwa manager bora (Wenger) na mchezaji bora (Ramsey) wa mwezi Septemba. Wenger na Ramsey wamepata tuzo hizi baada ya kuonesha ustadi mkubwa ndani ya klabu, kwani hadi sasa Arsenal inaongoza ligi ikiwa na point 16, na imeweza kuonesha mchezo safi wenye ushindani tofauti na miaka iliyopita. Tokea msimu huu uanze Wenger amekuwa akimpa nafasi Ramsey kwenye kikosi cha kwanza, na mchezaji huyu ameweza kuonesha kiwango cha hali ya juu tofauti na alivyokuwa akijulikana. Mbali ya kucheza kama kiungo na kuwasaidia washambuliaji, Ramsey amefanikiwa kufunga magoli manne hadi sasa.  

No comments:

Post a Comment