Monday, January 6, 2014

Azam yaingia robo fainali Mapinduzi Cup

Mechi kati ya Azam na Ashanti United imemalizika na Azam kushinda goli 1-0 lilipachikwa na Brian Umony kipindi cha pili cha.

Kwa ushindi huo Azam imeshinda michezo yote na kukusanya pointi zote tisa wakati Ashanti United wametolewa mashindanoni kwa kuzidiwa magopli ya kufunga na KMKM baada ya timu zote mbili (Ashanti na KMKM) kulingana kwa tofauti ya magoli ya kufunga nakufungwa. KMKM imefunga magoli mawili wakati Ashanti mefunga goli 1.

Baada ya timu nne zitakazocheza robo fainali kujulikana leo hatua hiyo ya nane bora itaanza keshokutwa Jumatano kwa kupigwa michezo miwili Pemba kwenye uwanja wa Gombani na miwili Unguja katika uwanja wa Amaan.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Kamati ya maandalizi ya Kombe la Mapinduzi, Tusker ya Kenya itacheza na URA ya Uganda katika mchezo wa kwanza huko Pemba kuanzia saa 8 mchana na kufuatiwa na mchezo wa pili kati ya Azam na Clove Stars saa 10 joini.

Michezo miwili itakayopigwa Unguja ni kati ya KCC na KMKM saa 10 na saa mbili usiku ni kati ya Simba na Chuoni ya Pemba.

Nusu fainali zote mbili zitapigwa Amaan Unguja Ijumaa Januari 10 kati ya mshindi wa mchezo wa Tusker na URA na ule wa Simba na Chuoni wakati nusu fainali ya pili itamkutanisha mshindi wa mchezo kati ya Azam na Cloves Stars na yule wa KCC na KMKM.

Robo fainali Mapinduzi Cup 

Tusker vs URA 
Simba vs Chuoni 
Azam FC vs Cloves Stars 
KCC vs KMKM 

No comments:

Post a Comment