Shirikisho la mpira wa miguu nchini Hispania limesema bado linafuatilia kitendo cha mchezaji wa Real Madrid Angel Di Maria kushika sehemu zake za siri wakati akitoka nje ya uwanja. Di Maria alifanya kitendo hicho kwenye mechi kati ya Real Madrid na Celta wakati akitoka uwanjani akiwa amefanyiwa mabadiliko dhidi ya Gareth Bale. Watu mbalimbali wakiwemo wachezaji wenzake pamoja na mkewe wamesema kitendo alichofanya Di Maria haikuwa makusudi na wala hakuwa anamfanyia mtu, bali ni kitendo cha kawaida kwa wachezaji kujiweka sawa. Lakini washabiki pamoja na waandishi wa habari wamekichukua kitendo hicho kama dharau au matusi dhidi ya watu au mtu fulani. Katika kuweka mambo sawa, klabu ya Madrid imesema itafanya uchunguzi wa jambo hilo na kulitolea ufafanuzi kwa kina ili kuondoa sitofahamu iliyopo kati ya washabiki na waandishi wa habari.
Video ya Di Maria akishika sehemu zake za siri
No comments:
Post a Comment