Friday, January 10, 2014

Tetesi za usajili leo tarehe 11 Jan 2014

Klabu ya Arsenal imeingiliwa na Benfica kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Morata. Klabu ya Arsenal ndiyo ilikuwa ya kwanza kusikika ikimhitaji Morata kwa mkopo kwenye dirisha dogo, lakini leo taarifa zinasema klabu ya Benfica inatoa ofa ya Euro 7 mil kwa Madrid ili kumsana mchezaji huyu. Ofa hiyo bado haijatolewa majibu lakini kama Madrid wataikubali basi klabu ya Arsenal itakuwa imemkosa mchezaji huyu. 

Marca linaripoti kuwa klabu ya Chelsea imekubali ofa iliyotolewa na Wolfsburg kumsajili Kevin de Bruyne kwa paundi mil 18. Taarifa zinasema kuwa aliyetoa ruhusa ya mchezaji huyu kuondoka ni Mourinho na muda wowote Wolfsburg itatangaza rasmi uhamisho wa mchezaji huyu. 

Mshambuliaji wa Tottenham na England, Jermain Defoe kujiunga na Toronto FC tarehe 28 February 2014

 
Raia wa Denmark na beki wa Liverpool, Daniel Agger ametajwa na vyombo vya habari kuwa mbioni kujiunga na Napoli ya Italia baada ya kushawishiwa na kocha wa zamani wa Liverpool Rafa Benitez. 

Out of time: Nemanja Vidic's Old Trafford career could be at an end in the summer after his agent ruled out a contract extension
Nemanja Vidic bado yupo kwenye headlines za vyombo vya habari kuhusu nia yake ya kutaka kuhama. Taarifa za leo kupitia Dailysport na Marca zinasema, klabu za Galatasaray na Barcelona ndiyo zimetajwa kutaka kumsajili mchezaji huyu. Lakini usajili wa mchezaji huyu umetajwa kuwa ni vigumu kufanyika kwenye dirisha dogo, kwani ni kipindi kifupi kwa United kutafuta mbadala wake, ila mchezaji huyu imesemekana atasaini mkataba wa awali na klabu moja wapo hadi hapo mkataba wake na Man utd utakapo malizika mwezi June 2014. 

Klabu ya Red Bulls ya Marekani imempa ofa kiungo wa Barcelona Xavi Hernandez kujiunga nao muda wowote akiwa tayari. Red Bulls imeshawishika kumsajili mchezaji huyu baada ya kuona kipindi chake cha kuitumikia Barcelona kimekaribia kuisha. Thierry Henry pia amekuwa ni mjumbe kwenye suala hili akiwa kama mshawishi mkubwa wa Xavi kujiunga na ligi ya Marekani. Mkataba wa Xavi na Barca unakwisha mwaka 2016. 

Wenger confident Rosicky will extend Arsenal contract
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo wa klabu hiyo Tomas Rosicky hatarajii kuondoka hata kama mkataba wake unakwisha baada ya miezi sita. Wenger amewahakikishia wapenzi wa Arsenal kuwa Rosicky bado anaipenda Arsenal na atasaini mkataba mpya muda sio mrefu. 

Messi: I want to finish my career at Barcelona
Baada ya tetesi za muda mrefu juu ya Lionel Messi kuwa anaweza kuhama Barcelona, mchezaji huyu amefunguka na kusema ataichezea Barca hadi mwisho wa maisha yake katika soka "Naipenda Barca, na natamani kuitumikia hadi mwisho, sina mpango wa kwenda klabu yoyote". Tetesi za Messi kutaka kuhama Barca zilivuma kipindi akiwa nchini Argentina akitibiwa mguu. Tetesi hizo zilitaja klabu za Manaco, Man city na PSG ndiyo zinamnyemelea mchezaji huyu. 

No comments:

Post a Comment