Monday, August 5, 2013

Juma Kaseja asajiliwa na FC Lupopo ya Kongo

Nahodha na Golikipa wa Taifa Stars, Juma Kaseja amesajiliwa na klabu ya FC Lupopo ya DRC kwa mkataba wa mwaka mmoja. Kaseja anatarajia kuondoka nchini wiki hii kuelekea Kongo ili kukamilisha uhamisho wake akiwa kama mchezaji huru. Kaseja alitemwa na klabu yake ya Simba mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake kuisha, na kumfanya awe mchezaji huru ambapo FC Lupopo watamsajili bila ada yoyote ya uhamisho.  

No comments:

Post a Comment