Thursday, January 9, 2014

Wachezaji nane wa Man utd wanatarajia kuuzwa

Wachezaji nane wa klabu ya Man utd wamesemekana wapo kwenye mpango wa kuuzwa kwenye dirisha dogo na mwishoni mwa msimu kutokana na nidhamu yao kuwa ndogo. Sportmail linahabarisha kuwa wachezaji hawa wamekuwa wakicheza chini ya kiwango tokea Moyes achukue timu na wanatuhumiwa kufanya mgomo wa chini chini. Kati ya hawa wachezaji nane, vinara wa mgomo wamesemekana kuwa ni Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra. 

Alipoulizwa Moyes kuhusu kiwango kidogo kutoka kwa wachezaji hawa alisema ' klabu ya Man utd kwa kipindi kirefu haijapitia hali iliyopo sasa baada ya Ferguson kuondoka. Wachezaji, viongozi na washabiki walishazoea uongozi wa Sir Alex hivyo itachukua muda kubadilika'. Majibu haya ya Moyes yalithibitisha ukweli kuwa wachezaji wanacheza chini ya kiwango ila hakuweza kuliongelea hili kwa uwazi zaidi. Ila wachambuzi wa soka pamoja na fununu zilizopo ndani ya klabu zinasema, wachezaji wengi bado hawajamkubali Moyes hali inayopelekea ka mgomo cha chini chini. Mbali ya Vidic, Ferdinand na Evra wachezaji wengine waliopo kwenye kapu la kuuzwa ni Javier Hernandez, Nani, Anderson, Alex Buttner and Anders Lindegaard. 

Robin Van Persie pia alikuwa aingie kwenye kundi hili la kuuzwa lakini ugeni wake ndani ya klabu na kuwa majeruhi kwa muda mrefu kumemfanya akae nje ya dimba kwa kipindi. Rooney pia ametajwa kucheza chini ya kiwango lakini matatizo ya Rooney na uongozi wa klabu yanajulikana kabla ya Sir Alex kuondoka. Kilio cha Rooney tokea enzi za Sir Alex ni kutaka kucheza nafasi ya ushambuliaji na sio nafasi ya kiungo. Hivyo mchezaji huyu bado yupo kwenye kundi la wachezaji wanaopendwa na Moyes na hadi sasa ameshapewa mkataba mwingine ili aongeza muda wa kuitumikia United. 

Suluhisho la matatizo yaliyopo ndani ya Man utd yanatarajiwa kupungua mwezi huu ikiwa Moyes atakubali kufanya usajili ili aweze kupata wachezaji wenye damu mpya. Wachezaji ambao hadi sasa wametajwa kuhusishwa na Man utd ni Fabregas,  Fabio Coentrao, Gundogan, Reus, Shaw na Diego Costa. 

Man utd kwasasa inashikilia nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 34 ambazo ni tofauti ya pointi 11 kutoka kwa kinara wa ligi klabu ya Arsenal. 

Ferguson akiwa na Vidic wakiangalia mchezo wa tenesi, wawili hawa bado ni marafiki, na mara kwa mara wanaonekana wakiwa pamoja. Hali hii ndiyo inafanya baadhi ya wachezaji kama Vidic waendelee kumkumbuka Sir Alex na kusahau kama muda huu wapo na Moyes  

No comments:

Post a Comment