Wednesday, August 7, 2013

Man utd wameanza maongezi na Marouane Fellaini

Time to go? Marouane Fellaini played on Tuesday night for Everton against Valencia
Sportsmail linaripoti kuwa Marouane Fellaini ndiye chaguo la Moyes baada ya Barcelona kugoma kumuuza Fabregas kwa Man utd. Ripoti zinasema tayari klabu ya Man utd imeshaanza maongezi na wakala wa mchezaji huyu anayechezea klabu ya Everton, klabu ambayo kocha wa sasa wa Man utd David Moyes alikuwa akiifundisha. Man utd inamuhitaji Fellaini ili aweze kuongeza nguvu kwenye nafasi ya kiungo ambayo inaonekana ni dhaifu baada ya Paul Scholes kustaafu. Fellaini anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Moyes, kwani klabu ya Everton na Fellaini mwenyewe tayari wameshaonesha nia ya kukubali ofa ya Man utd, ambayo itakuwa ni paundi mil 29 na mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki. 

No comments:

Post a Comment