Monday, January 13, 2014

Yanga waendelea na mazoezi nchini Uturuki

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Ankara Sekerspor, kaimu kocha mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa ameendelea kuwanoa vijana wake katika viwanja vya hotel ya Sueno Beach Side iliyopo pembeni kidogo ya mji wa Antalya katika eneo la mji wa Manavgat.

Kikosi cha wachezaji 27 kilichopo nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika kimeendelea na mazoezi kwa wachezaji wote na mpaka sasa hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja aliyekosa mazoezi hayo.

Mkwasa ametumia muda kidogo kabla ya kuanza mazoezi kuongea na wachezaji wake juu ya mchezo wa jana na kuelekezana makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo, kisha kuwapongeza vijana wake kwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake kitu ambacho kiliweza kuleta ushindi mzuri wa mabao 3-0.

Aidha Mkwasa amesema anandelea kukinoa kikosi na kuhakikisha vijana wanakua katika hali nzuri, kiakili, kiafya, morali na kifikra ili pindi watakaporejea nchini kwa ajili ya mzunguko wa pili basi timu iweze kuonekana ipo tofauti na mabadiliko katika kusaka ushindi.

Mkuu wa msafara wa Young Africans Salum Rupia amesema anashukuru tangu timu imefika nchini Uturuki wanaendelea vizuri na hakuna majeruhi wala tatizo lolote katika yao, kikubwa wanaendelea na mazoezi kwani ndo kitu kilichowaleta huku wakisubiri kucheza michezo miwili ya kirafiki inayoratibiwa na wenyeji na baada ya hapo timu itarejea nchini tayari kwa mzunguko wa pili. 

Video Yanga vs Ankara Sekerspor

No comments:

Post a Comment