Sunday, January 12, 2014

Tetesi za Usajili barani Ulaya terehe 13 Jan 14

Marca linahabarisha kuwa wachezaji watatu wa Man utd, Anderson, Nani na Zaha taratibu zao za uhamisho zipo kwenye hatua za mwisho na wanaweza kuhama muda wowote. Gazeti la Marca limemtaja kiungo Anderson anatarajia kwenda Fiorentina, wakati Nani atakwenda nyumbani kwao Ureno kuichezea Sporting Lisbon wakati Zaha akirudi kwa mkopo Cardiff City. Kuondoka wachezaji hawa ndiyo kunatarajiwa kutoa nafasi kwa United kufanya usajili wa wachezaji wengine ndani ya dirisha dogo. 

Mbali ya uongozi wa klabu ya Juventus kutangaza kuwa Paul Pogba hawezi kuuzwa ndani ya dirisha dogo, lakini mchezaji huyu bado anawindwa vilivyo na vigogo wa soka barani Ulaya. Wiki iliyopita Pogba alitajwa kutaka kusajiliwa na PSG, lakini wikiendi hii taarifa zimebadilika ambapo Man utd na Man city ndiyo zipo kwenye headlines za magazeti kutaka kumsajili mchezaji huyu. Uwepo wa kocha wa Man utd David Moyes kwenye mechi kati ya Cagliari vs Juventus kunaifanya klabu ya Man u kuwa kwenye hatua ya mbele kumsajili mchezaji huyu kuzidi Man city. 

Kuhusu Fabio Coentrao tayari vyombo vya habari nchini England na Spain vimeshaanza kutangaza uhamisho wa mchezaji huyu kwenda Man utd kwa mkopo. Magazeti ya Marca na Goal tayari yanasema Coentrao atahamia Man utd kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. 

Klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani tayari imethibitisha kuwa Kevin de Bruyne anahamia kwenye klabu hiyo ndani ya dirisha dogo. Kevin de Bruyne ambaye alikuwa akichezea  Werder Bremen kwa mkopo bado hajaweza kuonesha kiwango cha kutosha kuweza kumbakisha kwenye kikosi cha Chelsea tokea ajiunge mwaka 2012 akitokea Genk. Amekuwa akicheza kwa mkopo muda mrefu ndiyo maana klabu ya Chelsea imeamua kumuuza. 

Taarifa pia kutoka Uturuki zinasema klabu ya Galatasaray ipo mbioni kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria. Winga huyu amekuwa benchi mara kwa mara kutokana na changamoto ya namba kwenye kikosi cha kwanza, hivyo ametoa hamasa kwa klabu zingine kutaka kumsajili. Mbali ya Galatasaray pia klabu za Arsenal na Man utd zipo kwenye orodha. 

Gazeti la Diario de Noticias linathibitisha kuwa klabu ya Arsenal imetuma ofa ya paundi mil 12 ili kumsajili winga wa klabu ya Real Sociedad, Griezmann. Real Sociedad ni klabu iliyopata jina kubwa nchini Spain mwaka jana baada ya kufanya vyema hadi kupata nafasi ya kushiriki Uefa champions yote hii ni kwasababu ya kuwepo kwa wachezaji wenye viwango akiwemo Griezmann ndiyo maana klabu ya Arsenal imeshawishika kutaka kumsajili. 

Kiungo wa Chelsea Michael Essien yupo mbioni kwenda kwenye nyumba ya wazee klabu ya Ac Milan ndani ya dirisha dogo. Klabu ya Ac Milan ambayo ni maarufu kwa kusajili wachezaji wakongwe wameripotiwa na gazeti la La Gazzeta dello Sport la nchini Italia kutaka kumsajili mchezaji huyu ambaye pia ameonesha nia ya kutaka kuondoka Chelsea baada ya kusugua benchi kwa muda mrefu 

Tough: An exasperated David Moyes can't contain his frustration during the game at the Stadium of Light
Mtandao wa Goal UK unaripoti kuwa kocha mkuu wa Man utd amepatiwa jumla ya Euro 180 milioni kwa usajili wa dirisha dogo na mwisho wa msimu. Makubaliano haya yamefanywa kati ya Moyes, uongozi wa Man utd na mmiliki wa klabu familia ya Glazer. Makubaliano haya yametoa nguvu kwa Moyes kuweza kuunda kikosi chake lakini kwa mashariti kuwa klabu iweze kushiriki Uefa champions na kuchukua ubingwa ndani ya misimu miwili. Akishindwa kufanya hivi kibarua chake (Moyes) kitaota nyasi. 

No comments:

Post a Comment