Wednesday, April 3, 2013

Taribo West ameshikwa, alidanganya umri


Mchezaji wa zamani Taribo West imegundulika kuwa alidanganya umri wake kuwa ni miaka 28 wakati akiwa ana miaka 40. Taribo West Mnigeria ameshawahi kucheza katika club za Inter Milan, Derby County na Plymouth alimwambia raisi wa club ya Partizan ya Serbia kuwa ana umri wa miaka 28 wakati akiwa na umri wa miaka 40 akitokea Derby County kujiunga na Partizan. Zarko raisi wa Partizan alisema nilimsajili Taribo aliponiambia ana miaka 28, ila nilipogundua kanidanganya sikuweza kumfanya kitu kwasababu alikuwa anacheza mpira mzuri. West pia alihusishwa na tuhuma hizo za kudanganya umri alipokuwa Croatia kwenye club ya Rijeka alipomwambia daktari wa club hiyo kuwa ana umri wa miaka 32 badala ya miaka 44. Wachezaji wengi wa Afrika wamekuwa wakihusishwa na tuhuma za kudanganya umri sababu kubwa ikiwa ni ugumu wa maisha na afya njema ya kiafrika ambayo inamfanya Mwafrika aonekane mdogo hata akiwa mtu mzima. 

No comments:

Post a Comment