Thursday, February 13, 2014

Mchezaji wa Lazio na kashfa ya kudanganya umri

Age row: Lazio have threatened legal action after a youth team player, 17-year-old Joseph Minala was accused of being in his 40s. The club and his agent issued a statement rubbishing the claims
Klabu ya Lazio imeponda vikali kauli iliyotolewa na watu pamoja na gazeti la Senegal kuhusu umri wa mchezaji wake Joseph Marie Minala. Baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii pamoja na gazeti moja la Senegal wamesema kuwa Minala ana umri wa miaka 40 au zaidi tofauti na vyeti vyake vinavyosema kuwa ana miaka 17. Taarifa hizi zilianzia kwenye akaunti ya Minala ya Facebook baada ya watu 'kucomment' picha zake kwa kusema ana umri mkubwa jambo ambalo lilimfanya mchezaji huyu kuifunga akaunti yake ya facebook. Kufuatia taarifa hizi klabu ya Lazio anayochezea mchezaji huyu imesema itafungua kesi kwa gazeti lililodanganya umma kuhusu umri wa Minala. Lakini pia wakala wa mchezaji huyu bwana Diego Tavano amesema ni kweli sura ya Minala inaonekana ya mtu mzima kutokana na hali ya maisha magumu aliyokulia, lakini umri wake halisi wa sasa ni miaka 17. Kumekuwepo na taarifa za wachezaji wengi wa Afrika kudanganya umri wanapokwenda Ulaya ili waweze kupata ajira, tatizo hili ndiyo limepelekea watu kuhoji umri wa Minala jambo ambalo wakati mwingine linaweza kuwa la kweli au uongo. Ugumu wa maisha na kutafuta ajira kwa Waafrika ndiyo imekuwa sababu kuu ya kudanganya umri. Zifuatazo ni picha za Minala ambazo zinatiliwa shaka kwa kuwa na sura ya mtu mzima sio kijana wa miaka 17; 

 Documents: The club released official documents after Minala was the subject of abuse because of pictures he released on social networking sites - Minala has now deleted his Instagram and Facebook accounts
Goalscoring great: Minala pictured with Udinese hitman Antonio Di Natale
Storm: He was forced to delete his Instagram and Facebook accounts, but remains on Twitter
Joseph Minala

No comments:

Post a Comment