Thursday, February 13, 2014

Neymar amwagana na mpenzi wake Bruna

Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar amemwagana na mpenzi wake Bruna Marquezine baada ya kudumu kwenye mahusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja. Taarifa za kuachana kwa wapenzi hawa zilianza kusikika tokea mwaka mpya (1/1/2014) baada ya Neymar na Bruna kusherekea kila mtu kivyake nchini Brazil. Lakini taarifa za uhakika zimetoka wiki hii baada ya Bruna mwenyewe kuthibitisha kwa kutumia akaunti yake ya Instagram, na pia ameshazitoa picha zote akiwa na Neymar kwenye akaunti hiyo. Mbali ya instagram, Bruna pia alithibitisha kuachana na Neymar kupitia blog maarufu ya O Globo inayomilikiwa na Patrícia Kogut, ikiwemo pia taarifa kutoka gazeti la 'Samba Foot' lililoripoti kuwa tayari Bruna ameshaanzisha mahusiano mapya na kiungo wa klabu ya Flamengo, Mattheus Oliveira, na wameshatambulishana kwa wazazi. 

Lakini, kwa upande wa Neymar, yeye bado hajasema chochote kuhusu mahusiano yake, kwani wawili hawa wana mikataba mingi ya makumbuni mbalimbali wanayofanya matangazo pamoja. Neymar na Bruna walikuwa wakiishi wote nchini Hispania, lakini kwasasa kila mtu anaishi kivyake ambapo Neymar yupo Barcelona na Bruna anafanya kazi zake za muziki, filamu na urembo nchini Brazil. 


Picha mbalimbali za Neymar na Bruna 
Bruna akitoa machozi ya furaha siku ambayo Neymar alitambulishwa mbele ya umati wa watu kwenye uwanja wa Barcelona, Nou Camp. 

No comments:

Post a Comment