Wednesday, February 19, 2014

Shuti la mguu wa kushoto la Ibrahimovic ni hoja

Zlatan
Kumekuwa na maswali mengi ya kujiuliza baada ya Zlatan Ibrahimovic kufunga goli la tatu kati ya magoli manne ambayo PSG ilishinda dhidi ya Bayern Leverkusen. Kilichofanya goli hili kuibua maswali ni jinsi lilivyofungwa kwani Zlatan alipiga shuti kali lililomshinda golikipa wa Leverkusen kwa kutumia mguu wa kushoto ikiwa Zlatan mwenyewe hutumia mguu wa kulia kucheza. Kwa kawaida kila mchezaji huwa ana mguu ambao anatumia kucheza kama ni mguu wa kulia au kushoto. Wapo baadhi ya wachezaji wanatumia miguu yote, lakini lazima uwepo mguu mmoja ambao hutumika zaidi ya mwingine. Kwa upande wa Zlatan mguu wa kulia ndiyo anaotumia kucheza, lakini kiwango cha goli alilofunga dhidi ya Leverkusen kwa kutumia mguu wa kushoto kimeonesha uwezo wake mkubwa wa kutumia miguu yote kwa nguvu ile ile. Wachezaji wengi mashuhuri wa sasa akiwemo Ronaldo, Messi na Ribery hutumia miguu yote lakini kwa nguvu hafifu kwenye mguu wa pili, tofauti kabisa na ambavyo Zlatan ameonesha kwenye goli hili. Angalia video iliyopo chini ya goli alilofunga Zlatan kuthibitisha maneno haya;   

No comments:

Post a Comment