Monday, February 24, 2014

Sochi yaweka historia katika michuano ya Olimpiki

Michuano ya 22 ya Michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi yamekwisha jumapili hii mjini Sochi Urusi baada ya siku 17 za mashindano. Mashindano haya yaligharimu dola bilioni 30, ambazo ni fedha nyingi kupata kutokea katika historia ya mashindano ya Olimpiki duniani IOC. Rais wa shirikisho la Olimpiki duniani (IOC) Thomas Bach aliiambia dunia kuitizama Urusi kwa mtazamo mpya kwa mambo mengi tofauti na miaka iliyopita. Alisema wanaondoka Sochi wakiwa marafiki bila ya kumbukumbu ya changamoto zilizokuwepo awali. Bach Alisema Urusi aliyokuwa akiijua na kuisikia ni tofauti kabisa na alivyoiona mwaka huu katika kipindi chote cha mashindano, kwani ni taifa jipya na karimu mno. 

Zaidi ya wanariadha 2800 kutoka mataifa 88 walishiriki katika mashindano hayo yaliyojumuisha michezo 12 mpya. Urusi ilimaliza ya kwanza katika jedwali la medali ,ikiwa na medali 13 za dhahabu 11 za fedha na 9 za shaba. Norway ilimaliza ya pili na medali 11 za dhahabu 5 fedha na 10 za shaba. Canada ilikamilisha orodha ya tatu bora na jumla ya medali 10 za dhahabu 10 za fedha na 5 za shaba.

Baada ya kuiandalia dunia dhifa ya kukata na shoka , waandaaji wa mashindano ya Sochi waliwakabidhi wenzao Korea ya Kusini bendera ya kamati ya olimpiki. Mji wa Pyeong-chang ulioko Korea Kusini ndio utakaokuwa mwenyeji wa mashindano yajayo ya olimpiki ya msimu wa baridi mwaka wa 2018.

Baadhi ya matukio kwenye michuano ya Olimpiki Sochi 
Back of the net! Sweden goaltender Henrik Lundqvist can't stop a goal by Chris Kunitz during the third period

Masters: Canada's Ryan Fry looks down the rink after his team took an early lead against GB



No comments:

Post a Comment