Wednesday, February 5, 2014

Tetesi za usajili bado zinaendelea wiki hii Feb 5 licha ya dirisha dogo kufungwa

Class performer: Sagna, seen here holding off Borussia Dortmund's Henrikh Mkhitaryan and Marco Reus, right, helped Arsenal beat the German side 1-0 in the Champions League group stages earlier this season
Beki wa kulia wa Arsenal, Bacary Sagna anatarajia kupewa mkataba mwingine na klabu ya Arsenal baada ya kukataa kusaini mikataba miwili. Mkataba wa sasa wa Sagna unatarajia kuisha mwishoni mwa msimu na klabu ya Arsenal haipo tayari kumuachia mchezaji huyu kuondoka kama mchezaji huru. Sagna aligoma kusaini mikataba miwili aliyopewa na Arsenal kwasababu ina maslahi madogo na muda wake ni mfupi. Taarifa kutoka Sportsmail zinasema Sagna anahitaji mkataba mrefu wa miaka mitatu au minne pamoja na kuongezewa malipo yake kwa wiki yawe zaidi ya paundi 60,000. Mbali ya maslahi, Sagna pia aligoma kusaini mikataba aliyopewa awali kwasababu anajua umri wake umeshakwenda, hivyo angependa kupata mkataba wa muda mrefu ili amalizie kazi yake akiwa na Arsenal. Klabu tatu zimeshaonesha nia ya kutaka kumsajili Sagna kama Arsenal itashindwa kutimiza mahitaji yake, klabu hizo ni PSG, Monaco na Galatasary. 

 Is he Gunner go back? Arsenal manager Arsene Wenger admits he would have Cole in his team again
Baada ya kusugua benchi kwa muda mrefu, taarifa zimeanza kuzagaa kuwa beki wa kushoto wa Chelsea, Ashley Cole anaweza kurudi tena Emirates kujiunga na klabu yake ya zamani Arsenal. Sportsmail limesema Cole amekuwa kwenye wakati mgumu tokea Mourinho arudi Chelsea na amekuwa akimpanga Azpilicueta badala yake. Cole alishatangaza kuwa anafikiria kustaafu ila hadi afikie kiwango cha kushindwa kucheza kiushindani. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alishaulizwa kuhusu habari za Cole kutaka kurudi Arsenal na alisema ' muda ukifika nikiwa nahitaji beki wa kushoto nitamsajili'. Kauli hii ya Wenger imempa nguvu Cole na inawezekana akarudi Emirates mwishoni mwa msimu. 

Onlooker: Cole has spent more time than he'd like on the sidelines this season under Mourinho
Cole akiwa benchi kwenye mechi kati ya Man city na Chelsea

Target: Manchester United have been watching Sporting Lisbon's William Carvalho
Klabu ya Man Utd imeonesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho. Taarifa hizi zimetolewa na jarida la Ureno 'O Jogo' baada ya ujumbe wa Man utd kutua jijini Lisbon wikiendi hii kuongea na wakala wa mchezaji huyu na kushiriki kwenye mechi kati ya Sporting na Academica, mechi iliyokwisha kwa droo ya bila kufungana. Taarifa zinasema Moyes ameshamkubali mchezaji huyu na United inataraja kumsajili mwisho wa msimu kabla ya kombe la dunia. Carvalho anachezea pia timu ya taifa ya Ureno na alionesha uwezo mkubwa kwenye hatua za kufuzu kombe la dunia wakati Ureno ilipoitoa Sweden. 

Staying? John Terry could be about to sign a one-year contract extension with Chelsea
Beki wa Chelsea John Terry imebidi akubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake baada ya kujulishwa sheria za Chelsea. Terry alikuwa anahitaji kusaini mkataba wa miaka mitatu, lakini klabu iligoma kumpa mkataba wa muda mrefu kwasababu sheria za klabu ya Chelsea zinasema mchezaji anayezidi miaka 30 anatakiwa kupewa mkataba wa miezi 12 tu. Terry kwasasa ana umri wa miaka 33 na mkataba wake unakwisha mwezi June mwaka huu hivyo anatakiwa kusaini mkataba mpya kabla msimu haujaisha. Mkataba mpya atakaosaini Terry utamfanya aongezewe malipo zaidi ya paundi 150,000 kwa wiki anayopata hivi  sasa.  Awali Terry aligoma kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kwa kutokujua sheria za klabu na kutaka kwenda USA kujiunga na Galaxy

Bayern: We won't sell Kroos to Man Utd
Klabu ya Bayern Munich imepigilia msumari wa uhakika kuthibitisha kuwa Kroos hawezi kuondoka ndani ya klabu hiyo hadi mkataba wake utakapokwisha. Taarifa hizi zimetolewa na Matthias Sammer ambaye ni mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich akisema ' Kroos hawezi kuuzwa kwenda Man utd, haikuwezekana kuondoka January na mwisho wa msimu pia hawezi kuondoka. Bayern Munich ni klabu inayonunua wachezaji sio kuuza. Kroos ameshatoa ahadi kwa kocha wake Pep kuwa hana mpango wa kuhama na sisi hatuwezi kukubali aondoke hadi mwaka 2015 mkataba wake utakapokwisha'. Kauli hii ya Bayern imebadilisha mawazo ya Moyes ambaye alitaka kumsajili kiungo huyu wakati wa dirisha dogo. Moyes alishafikia hatua ya kukutana na wakala wa Kroos nchini Ujerumani lakini makubaliano yao yameshaingia dosari. 

Kiungo wa Man utd, Anderson aliyesajiliwa kwa mkopo na Fiorentina amesema anataka kuendelea kubaki nchini Italia kwa mkataba mrefu. Kiungo huyu ameongea hayo na The Sun akisema ' ninafuraha kuwepo Fiorentina, ni klabu nzuri. Sina mpango wa kutaka kurudi tena Man utd, ninachohitaji ni kupewa kibali cha kucheza Italia kwa muda mrefu. Sio kwamba United ni klabu mbaya kwangu, ila ningependa kubaki huku. Nimeishi vizuri na Moyes na familia ya United lakini kwasasa nipo Italia na nitapenda kuendelea kuichezea Fiorentina'. 

Kocha wa Chelsea amethibitisha kuwa mwishoni mwa msimu atasajiri mshambuliaji wa kati mwenye uzoefu. Taarifa hizi zimetolewa na Skysport zikisema 'Mourinho ana mpango wa kusajili mchezaji mpya wa mbele lakini hajasema ni mchezaji gani atamsajili. Ila kwa habari zilizopo ndani ya klabu ni kwamba wachezaji watatu ndiyo wapo kwenye kichwa cha Mourinho ambao ni Cavani, Mario Mandzukic na Diego Costa'. Taarifa za awali kutoka Marca nchini Hispania zinasema tayari Chelsea na Atl. Madrid zimeshakubalina kuhusu Diego Costa kuhamia darajani mwisho wa msimu. Ila mkataba huo sio wa uhakika asilimia 100 hivyo klabu ya Chelsea inajipanga kutafuta wachezaji wengine ili dili la Costa likigoma wawe na mbadala. 

No comments:

Post a Comment