Thursday, February 13, 2014

Usain Bolt aiponda Arsenal baada ya droo Emirates

Bingwa wa mbio fupi duniani Usain Bolt ambaye pia ni shabiki mkubwa wa klabu ya Man utd, ameiponda waziwazi klabu ya Arsenal kupitia akaunti yake ya Twitter. Bolt aliandika kwamba 'acha historia iwepo kuwa Arsenal ilishindwa kuifunga Man utd mbovu'. Bolt alitoa kauli hii baada ya mchezo wa jana kuisha kwa droo ya 0-0 kati ya Arsenal na Man utd. Washabiki wengi wa soka walitarajia kuwa Arsenal ingeweza kushinda kwenye mchezo wa jana, lakini Man utd waliweza kuwabana Arsenal jambo ambalo limeshangaza wengi kutokana na ukweli kuwa Man utd ya msimu huu ni mbovu. Picha iliyopo chini ndiyo Tweet ya Bolt kuhusiana na kauli yake dhidi ya Arsenal. 

BgTiVLOIIAAJxEx Man United fan Usain Bolt mocks Arsenal on Twitter, Piers Morgan swiftly reminds him of league position

No comments:

Post a Comment