Sir Alex Ferguson (katikati) akiwa amesimama na viongozi wa chuo cha Ulster Ireland baada ya kupewa degree ya heshima kutokana na mchango mkubwa aliyoutoa kwenye soka hususani Man utd. Katika maneno yake mbele ya wanachuo 500 Sir Alex alisema ' Najivunia kupokea degree hii ya heshima kutoka kwenye chuo kikubwa kama hiki. Ninayo furaha sana kuona hata chuo kimeona mchango wangu na kufikiria kunipa tuzo. Hii ni ishara tosha kuwa mafanikio yangu katika soka yatawahamasisha pia wanachuo ambao wana ndoto ya kutimiza mambo makubwa kwenye maisha yao kwa kudumisha yale niliyokuwa nayaamini kama chachu ya mafanikio ambayo ni bidii na tabia njema'.
No comments:
Post a Comment