Tuesday, April 15, 2014

Kauli ya meneja wa Azam FC kuhusu ubingwa

"Maneno yanayozungumzwa ni porojo Baada ya Azam Fc kupata mafanikio ya kuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Azam Fc ilipata nafasi ya pili mara Mbili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara haikuwai kusemwa imenunua leo iweje imekuwa Bingwa isemwe imenunua.

John Bocco ameweka Historia Baada ya Kufunga Goli la Ushindi ktk Mechi ya Mwisho ya Ligi Daraja la kwanza na Kuipandisha Azam Fc kucheza Ligi kuu ya Tanzania Bara, na leo Hii Tumeshuhudia John Bocco ameweka Historia ya Kufunga Goli la Ushindi na Kuipa Timu ya Azam Fc Ubingwa kwa Mara ya kwanza Tangu ilipopanda Daraja kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara kwa Msimu 2013/2014 na kucheza Bila kupoteza hata mechi Moja.

Hatuto puuzia mechi ya mwisho Dhidi ya JKT Ruvu Tutacheza kama mechi nyingine Tulivyocheza Tunahitaji kuweka Historia ya Kutokupoteza hata Mechi Moja kwa Msimu Huu JKT Ruvu wajiandae kwa Kichapo wakati Tukiwa Tunakabidhiwa Kombe letu la Msimu Huu

Baadhi ya Maneno ambayo Makocha wanazungumza Sio Mazuri wao kama wataalam hawatakiwi kujihusisha katika Propaganda ambazo baadhi ya watu wanaziendeleza".

Ni maneno ya Jemedari Said meneja wa Azam fc pamoja na Katibu Mkuu Nassoro Idrisa 

No comments:

Post a Comment