Kocha wa Man
City Roberto Mancini amechukizwa na kitendo cha kocha wa Belgium Marc Wilmots
kumchezesha beki wa Man City Vicent Kompany. Mancini akiongea na BBC sport
amesema, Kompany ameondoka hapa bado hajapona na hajacheza mechi yoyote toka
January, lakini yeye Wilmots amemchezesha dakika zote 90 bila kuomba ushauri
kwa madaktari wa Man City, nafikiri baadhi ya makocha wa timu za taifa lazima
waelewe kuwa hawa wachezaji ni wanadamu pia. Kompany ameondoka hapa akiwa bado
hajapona inawezekanaje ndani ya wiki moja awe amepona? alihoji Mancini. Kompany
aliumia mwezi wa kwanza kwenye ya FA kati ya Man city na Stoke.
No comments:
Post a Comment