Mario na Fanny |
Mshambuliaji wa Ac Milan Mario Balotelli ameweka wazi siri
ya mafanikio yake baada ya kuhamia nchini Italy akitokea England (Man City).
Balotelli amesema kwasasa yupo kwenye mapenzi mazito sana na Fanny “ ni kweli
kiwango changu kimepanda, sababu kubwa ni Fanny mpenzi wangu wa sasa, nampenda
sana, amefanya maisha yangu yabadilike, naweza kuishi naye maisha yangu yote
duniani, namshukuru sana Fanny, ameyaweka mapenzi yetu mbele, hakuna jambo linaloweza kuingilia mapenzi yetu, ki-ukweli Fanny ndiye
aliyenifanya nibadilike maisha yangu ya ndani na nje na kiwanja. Mario Balotelli aliyehamia Ac
Milan kutoka Man City kwa paundi milioni 19 ameshacheza mechi sita na kufunga
magoli saba.
No comments:
Post a Comment