Kiungo wa Barcelona Xavi alitimiza ahadi aliyopewa na Miquel
ambaye ni kijana wa miaka 10 anayeugua kansa. Xavi alikutana na kijana huyo
hospitali moja nchini Hispania na kijana huyo alimwomba Xavi vitu viwili, cha
kwanza aliomba kushiriki kwenye mazoezi ya Barcelona siku atakapo pata nafuu na
jambo la pili alimwomba Xavi ashike kichwa chake akifunga goli lolote kwa
Barcelona. Siku ya jumanne Xavi alitimiza ahadi hiyo kwa kijana Miquel baada ya
kufunga goli dhidi ya PSG na kushika kichwa chake huku akishangilia kwa furaha.
Xavi mwenyewe amesema anaamini Miquel atakuwa amefarijika na anamwombea nafuu
ya haraka. Xavi ni mfano mzuri kwa wanamichezo wa bongo, ni jambo jema kuwafariji wagonjwa na watu wenye mahitaji sio lazima kuwapa pesa.
Xavi aliposhika kichwa kutimiza ahadi baada ya kufunga goli dhidi ya PSG |
No comments:
Post a Comment