Goli la Luis Suarez lilifungwa dakika ya 95 ya mchezo
limeongeza ushindani wa kuwania nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa ligi kuu
nchini Uingereza baada ya Chelsea kutoka sare ya goli 2-2 dhidi ya Liverpool. Kwa
matokeo ya leo Chelsea wamebakia nafasi ya nne wakiwa na pointi 62 wakati
Arsenal ipo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 63 na Tottenham nafasi ya tano pointi 61. Liverpool wenyewe wamefikisha pointi 51 wakiwa nafasi ya saba nyuma
ya Everton yenye pointi 56. Magoli ya Chelsea yamefungwa na Oscar dk ya 26 na
Hazard dk ya 57 (penati) na yale ya Liverpool yamefungwa na Sturridge dk 52 na
Suarez dk ya 95.
|
Kocha wa Chelsea Rafa Benitez akiwapungia mkono mashabiki wa
Liverpool walipokuwa wanamshangilia kwa furaha baada ya kuingia uwanjani leo
wakati Chelsea ilipokutana na Liverpool. Benitez amepewa mapokezi hayo mazuri
na mashabiki wa Liverpool ikiwa ni shukrani kwake akiwa kama kocha aliyeipa
mafanikio makubwa Liverpool ikiwemo kombe la UEFA champions mwaka 2005.
|
No comments:
Post a Comment