Klabu ya Yanga leo imendelea kuusogelea ubingwa baada ya kushinda goli tatu kwa bila dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika jijini Dar es salaam. Goli la kwanza la Yanga lilifungwa na Saimon Msuva katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza na hadi mapumzika Yanga 1 - 0 JKT. Kipindi cha pili kilianza na kasi kwa timu zote lakini walikuwa Yanga tena kupitia kwa Hamis Kiiza aliyefunga goli la pili katika dakika ya 59 ya mchezo kabla ya Nizar Khalfani kumalizia kitabu cha magoli kwa kufunga goli la tatu katika dakika ya 65. Kwa matokeo haya Yanga imefikisha pointi 56 na imebakiza pointi moja tu ili kutangazwa mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2012/2013.
No comments:
Post a Comment