Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Jamhuri Kiwelu Julio amesema Simba
wamekubali kukosa nafasi ya kwanza na ya pili kwenye ligi ya mwaka huu na
kwasasa wanacheza kulinda heshima ya klabu hiyo. “Kwasasa Simba tunacheza
kujenga heshima, ila sio kuwania nafasi yoyote kwenye ligi, lakini tumeshaanza
kujipanga kwa ajili ya msimu ujao, kuna mapungufu madogo madogo tunarekebisha
kwa ajili ya msimu ujao”. Kiwelu aliyasema hayo baada ya mchezo wa jumapili
kulazimishwa sare ya goli 2-2 na Azam FC kwenye uwanja wa taifa jijini
Dar es salaam. Simba ambayo ni mabigwa wa mwaka jana ipo nafasi ya nne kwenye
msimamo wa ligi nyuma ya Kagera Sugar iliyopo nafasi ya tatu na pointi 40, wakati kinara wa ligi Yanga wana pointi 56 na Azam FC ipo nafasi ya pili pointi
47. Yanga na Azam FC ndiyo timu zitakazo iwakilisha Tanzania katika michuano ya
kimataifa mwakani barani Afrika.
No comments:
Post a Comment