Liverpool wamethibitisha kwenda nchini Thailand kwenye
mechi ya kirafiki baada ya msimu kuisha. Liverpool katika ziara yao watacheza
na timu ya taifa ya Thailand kwenye uwanja wa Rajamangala uliopo jijini Bangkok
tarehe 28 mwezi wa saba. Pamoja na mechi hiyo, Liverpool wakiwa Thailand pia
watafanya shughuli zingine za kijamii na kitalii. Thailand ni moja kati ya nchi
zenye washabiki wengi wa Liverpool duniani wakikadiriwa kufikia milioni 10, idadi hii ya mashabiki ndiyo sababu mojawapo ya Liverpool kwenda nchini humo ili kuimarisha mahusiano na
washabiki na kuitangaza Standard Chartered.
No comments:
Post a Comment