Kiungo wa Arsenal, Ramsey amesema sababu kubwa iliyomfanya
ajiunge na Arsenal na kuikacha Man Utd ni juhudi alizoonesha kocha wa Arsenal
Arsene Wenger na mahusiano mazuri na wachezaji yalipo kwenye club hiyo. Ramsey
alisema “ kocha Wenger alituma ndege binafsi kutoka London hadi Wales
nilipokuwepo ili inichukue niende kuongea naye, nilipofika walinipokea vizuri
na kunipeleka kwa Wenger ambapo alinipa mipango mizuri ya kukuza kipaji changu”. Mambo haya mawili ndiyo yalinifanya nije Arsenal na kuiacha
United, kwani sikuwahi kufikiria kama club kubwa kama Arsenal inaweza kunitumia
ndege binafsi na vilevile nilivutiwa sana na mipango mizuri niliyopewa na
Wenger. Ramsey (22) alijiunga na Arsenal mwaka 2008 ameshacheza mechi 96 na magoli 7.
No comments:
Post a Comment