Kikosi cha timu ya Young Africans Sports Club leo kimeanza tena mazoezi baada ya kuwa na mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa mabatini Kijitonyama, kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya timu ya JKT Oljoro kutoka jijini Arusha mchezo utakaofanyika Aprili 10 2013. Young Africans ambayo mwishoni mwa wiki ilitoka suluhu ya bila kufungana na timu ya Polisi Morogoro, bado inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na poniti 49, zikiwa ni ponti sita (6) mbele ya timu ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 43, Yanga inahitajika kushinda michezo mitatu ilyobakia ili kujihakikishia ubigwa kama Azam ataendelea kushinda michezo yake iliyobakia. Yanga imebakisha jumla ya michezo mitano (5) ili kukamilisha michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013, michezo iliyobaki ni kama ifuatavyo:
Aprili 10, 2013 : Young Africans Vs JKT Oljoro (Uwanja wa Taifa - Dar es salaam)
Aprili 13, 2013 : Mgambo Shooting Vs Young Africans (Mkwakwani - Tanga)
Aprili 21, 2013 : JKT Ruvu Stars Vs Young Africans (Uwanja wa Taifa - Dar es salaam)
May 01, 2013 : Young Africans Vs Coastal Union (Uwanja wa Taifa - Dar es salaam)
May 18, 2013 : Simba SC Vs Young Africans (Uwanja wa Taifa - Dar es salaam)
No comments:
Post a Comment