Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi watakaochezesha mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na Barrack Young Controllers II ya Liberia itakayochezwa Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mwamuzi wa kati ni Adelaide Ali, mwamuzi msaidizi namba moja ni Amaldine Soulaimane wakati Ibrahim Mohame atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ansudane Soulaimane. Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni atakuwa Abdelhamid Radwan kutoka Misri. Maofisa hao wa mechi hiyo watafikia kwenye hoteli ya Holiday Inn.
No comments:
Post a Comment