Wajumbe
wa FIFA wanatarajiwa kufika nchini April 16 mwaka huu kutathimini na kutolea
maamuzi mgogoro ulioibuka ndani ya TFF kuhusu uchaguzi mkuu. Ndolanga ambaye ni
mjumbe wa kudumu wa shirikisho hilo amesema ataeleza ukweli wote kuhusu
matatizo yaliyopo TFF. Ndolanga alisema, wao kama TFF watahojiwa na sisi kama
wadau tutahojiwa, ikifika zamu yangu nitaeleza ukweli wote bila kuficha,
"haiwezekani TFF wafanye madudu na sisi tukae kimya". Ndolanga
aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, lakini hakutaka
kusema ni mambo gani atawaeleza FIFA.
No comments:
Post a Comment