Mchezaji wa zamani Taribo West imegundulika kuwa alidanganya
umri wake kuwa ni miaka 28 wakati akiwa ana miaka 40. Taribo West Mnigeria
ameshawahi kucheza katika club za Inter Milan, Derby County na Plymouth
alimwambia raisi wa club ya Partizan ya Serbia kuwa ana umri wa miaka 28 wakati
akiwa na umri wa miaka 40 akitokea Derby County kujiunga na Partizan. Zarko
raisi wa Partizan alisema nilimsajili Taribo aliponiambia ana miaka 28, ila
nilipogundua kanidanganya sikuweza kumfanya kitu kwasababu alikuwa anacheza
mpira mzuri. West pia alihusishwa na tuhuma hizo za kudanganya umri alipokuwa
Croatia kwenye club ya Rijeka alipomwambia daktari wa club hiyo kuwa ana umri wa
miaka 32 badala ya miaka 44. Wachezaji wengi wa Afrika wamekuwa wakihusishwa na tuhuma za kudanganya umri sababu kubwa ikiwa ni ugumu wa maisha na afya njema ya kiafrika ambayo inamfanya Mwafrika aonekane mdogo hata akiwa mtu mzima.
No comments:
Post a Comment